Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 15, 2024 Local time: 02:50

Uturuki: Usafirishaji wa chakula kutoka Ukraine ni lazima uendelee


Meli ya kubeba chakula kutoka Ukraine ikisubiri kupita Yenikapi, Istanbul, Uturuki. Oct, 31, 2022
Meli ya kubeba chakula kutoka Ukraine ikisubiri kupita Yenikapi, Istanbul, Uturuki. Oct, 31, 2022

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema kwamba nchi yake inajaribu kwa njia zote kutumikia biandamu na kuendelea kuhakikisha kwamba makubaliano ya kusafirisha chakula kutoka Ukraine yanaendelea kutekelezwa.

Makubaliano hayo yalipatikana baada ya mazungumzo yaliyosimamiwa na Umoja wa mataifa na Uturuki, na kuruhusu tani milioni 9 za nafaka kuondoka bandari za Ukraine.

Russia ilitangaza jumamosi kwamba ilikuwa inasitisha mkataba huo, ikidai kwamba Ukraine ilikuwa imeshambulia meli zake katika bahari ya black sea, madai ambayo Ukraine imekanusha.

Bila kutoa ufafanuzi zaidi, Erdogan amesema kwamba Russia inasita kutekeleza mkataba huo kwa sababu haioni faida zake jinsi inavypata Ukraine.

"Ushirikiano wa pamoja tulioanzisha Istanbul, ulipelekea kupunguza ukosefu wa chakula duniani kwa kuwezesha tani milioni 9.3 za chakula kuingia katika soko la kimataifa. Japo Russia inasita kuendelea kutekeleza mkataba huo kwa sababu inaona kama haipati fursa sawa na inazopata Ukraine, tutaendelea na juhudi zetu kwa ajili ya ubinadamu."

Russia imesema kwamba itakuwa hatari kwa Ukraine kuendelea kusafirisha nafaka kupitia bahari ya black sea, ikitiliwa maanani kwamba utawala wa Moscow umejiondoa kwenye makubaliano hayo yaliyosimamiwa na umoja wamataifa kufanikisha usafirishaji wa nafaka.

Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov, ameambia waandishi wa habari kwamba Russia inazungumzia kuhusu kutohakikisha kwamba meli zinazofasirisha nafaka zitakuwa salama.

Licha ya taarifa ya Russia, meli za kusafirisha nafaka zimeondoka bandari za Ukraine leo jumatatu, zikiwa zimebeba tani 30,000 za ngano, baadhi zikielekea pembe ya Afrika ambako kuna uhaba mkubwa wa chakula kutokana na ukame.

Wizara ya ulinzi ya Uturuki imesema kwamba mazungumzo yanaendelea kuhakikisha kwamba mkataba wa usafirishaji wa nafaka unaendelea kutekelezwa.

XS
SM
MD
LG