Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 16:45

Tanzania na Uturuki zaafiki baraza la pamoja la uchumi


Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan
Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan

Taasisi ya sekta binafsi Tanzania (TPS) na bodi ya mahusiano ya kigeni kwenye masuala ya kiuchumi nchini Uturuki wameingia makubaliano ya kuanzisha baraza la kibiashara baina ya nchi hizo mbili.

Kwa mujibu wa mwandishi wa idhaa ya Kiswahili VOA, Dina Chahali lengo la kuanzisha baraza hilo ni kusaidia kukuza biashara kati yao ikiwa ni matokeo ya ziara ya rais wa Uturuki nchini Tanzania RecepTayip Erdogan.

Rais wa Uturuki, pamoja na mambo mengine, wakati wa ziara yake alisaini mikataba tisa ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya sekta binafsi, Godfrey Simbeye amesema ni wakati sasa kwa wafanyabiashara hapa nchini kuchangamkia fursa ambazo zinajitokeza hususan zinazotolewa na wafanyabiashara kutoka nje ili kukuza uchumi wa nchi.

Amesema baraza hilo waliloingia makubaliano jana na serikali ya Uturuki litaweza kutambua changamoto za kibiashara baina ya nchi hizo mbili.

Aliongeza kuwa litaleta ushirikiano kiuchumi na kutoa mapendekezo ya jinsi gani serikali husika zitakavyo zitatua na pia kuwawezesha wajasiriamali wadogo na wa kati kwa pamoja kuwapa ujuzi na maarifa.

Taasisi ya sekta binafsi Tanzania ndio itakuwa na jukumu la kuhakikisha kunakuwa na ufuatiliaji katka kufanikisha biashara baina ya Tanzania na Uturuki

Rais Erdogan katika hotuba yake jana jijini Dar es salaam alisisitiza kwamba sera ya Uuruki kwa Afrika ni usawa sio kunufaisha upande mmoja hivyo kupitia serikali yake wanataka kuleta maendeleo na kuliunganisha bara la Afrika


Imetayarishwa na mwandishi wetu Dina Chahali, Tanzania

XS
SM
MD
LG