Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 24, 2023 Local time: 17:04

Mshambuliaji wa klabu ya usiku mjini Istanbul bado anatafutwa


Waziri mkuu wa Uturuki, Binali Yildrim akiongea na majeruhi mmoja wa shambulizi kwenye klabu ya usiku mjini Istanbul.

Kuna taarifa zimetufikia, lakini serikali wanaendelea kupata ukweli kamili, Yildrim aliwaambia waandishi wa habari Jumapili jioni.

Mtu mwenye silaha ambaye ameua watu 39 kwenye kklabu ya usiku mjini Istanbul mapema Jumapili anaendelea kusakwa na vyombo vya usalama vya Uturuki.

Lakini waziri mkuu wa Uturuki, Binali Yildrim amesema vyombo hivyo mpaka hivi sasa 'havina uhakika' nani aliyehusika na shambulio hilo.

"Kuna taarifa zimeanza kutufikia, lakini serikali wanaendelea kupata ukweli kamili," Yildrim aliwaambia waandishi wa habari Jumapili jioni.

Hakukuwa na upande wowote uliodai kuhusika na shambulizi hilo katika nyumba hiyo ya starehe ambayo ilikuwa imejaa watu waliokuwa wanasherehekea mwaka mpya.

waziri wa mambo ya ndani wa Uturuki, Suleyman Soylu na Vasip Sahin, Gavana wa Istanbul, wamesema shambulizi hilo katika klabu ya usiku lilitekelezwa na mtu mmoja mwenye silaha.

Katika wale ambao wametambuliwa katika mauaji hayo 15 kati yao ni wageni. watano ni waturuki, Soylu amesema. Watu 18 bado hawajaweza kutambuliwa.

Soyulu amesema watu 69 wanatibiwa hospitali kutokana na majeraha, wanne kati yao wako katika hali mbaya na mmoja yuko mahututi.

Gavana ameliita tukio hilo ni shambulizi la kigaidi. Amesema mshambuliaji huyo ametumia silaha yenye mtutu mrefu kuwaua kinyama na kikatili watu waliokuwa wakisherehekea sikukuu ya mwaka mpya.

"Magaidi hawa wanajaribu kuleta mvurugano, kuwavunja moyo wananchi, na kuiyumbisha nchi yetu kwa mashambulizi ya kinyama ambayo yanawalenga wananchi," Rais Recep Tayyip Erdogan amesema.

"Tutaendelea kutumia busara kama taifa, tukishikamana zaidi na hatutatoa fursa kwa michezo hii michafu," amesisitiza rais.

Polisi wa Uturuki tayari wamelizunguka eneo karibu klabu hiyo ya starehe linaloitwa Reina ambako shambulizi lilitokea na kuongeza ulinzi kwenye eneo la Ortakoy, sehemu nyingine ya burundi katika eneo la Bosporus ambalo ni maarufu kwa kuwa na masupasta na wageni.

XS
SM
MD
LG