Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 07, 2024 Local time: 00:06

Vyombo vya habari vya Uturuki vyaonyesha video ya 'Selfie" ya mshukiwa

Afisa polisi wa Uturuki anaangalia picha za waathirika wa shambulizi la kwenye klabu ya usiku, Istanbul. Januari 2, 2017.
Afisa polisi wa Uturuki anaangalia picha za waathirika wa shambulizi la kwenye klabu ya usiku, Istanbul. Januari 2, 2017.

Mshukiwa alipokuwa akipiga picha hiyo alionekana kutumia muda mwingi kujipiga picha mwenyewe, lakini alikuwa haongei chochote.

Vyombo vya habari nchini Uturuki vimeonyesha kanda ya video ya mtu anayeshukiwa kuwa ndiye mtuhumiwa aliyetumia bunduki kuua watu 39 katika sherehe za mwaka mpya kwenye klabu ya usiku mjini Istanbul.

Video hiyo inaelekea ilipigwa kutoka katika simu ya mkononi wakati mshukiwa huyo akizunguka kwenye eneo la Taksim Square mjini Istanbul.

Mshukiwa alipokuwa akipiga picha hiyo alionekana kutumia muda mwingi kujipiga picha mwenyewe, lakini alikuwa haongei chochote.

Haijajulikana mpaka hivi sasa lini video hiyo ilirekodiwa.

Vyombo vya dola hapo awali vilitoa picha iliyokuwa si nzuri ya mshambuliaji huyo kutoka katika mkanda uliorekodiwa na kamera za ulinzi.

Vyombo vya habari vya Uturuki viliripoti Jumanne kwamba polisi wamewakamata raia wawili wa kigeni katika uwanja wa ndege wa Ataturk kuhusiana na shambulizi hili. Lakini hakuna taarifa za ziada zilizotolewa.

Waziri mkuu wa Uturuki, Numan Kurtulmus amewaambia waandishi wa habari Jumatatu kwamba watu wengine wanane wanashikiliwa na polisi.

XS
SM
MD
LG