Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Februari 27, 2024 Local time: 02:02

Rais Suleyman Demirel aaga dunia.


 Rais Suleyman Demirel kwenye picha ya awali.
Rais Suleyman Demirel kwenye picha ya awali.

Rais wa zamani wa Uturuki Suleyman Demirel na ambaye ni miongoni mwa viongozi mashuhuri wa nusu karne iliyopita ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 90. Madaktari kwenye hospitali ya Guven iliyoko Ankara wametangaza kifo cha kiongozi huyo Jumatano. Bw Demirel amekuwa akiugua ugonjwa wa kupumua. Bw Demirel aliingia madarakani katika miaka ya 60 na akaongoza kwa mihula mitano akiwa waziri mkuu kabla ya kuwa rais kuanzia 1993 hadi 2000. Alipinduliwa na jeshi mara mbili kwanza 1971 na kisha 1980, lakini akaweza kurudi madarakani kama waziri mkuu,1991 na hatimaye kuwa rais.

XS
SM
MD
LG