Akizungumza katika kikao na waandishi wa habari mjini Ankara, Uturuki, akiwa na waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Mevlüt Çavuşoğlu, Stoltenberg amesema kwamba suala kubwa sio iwapo nchi hizo mbili zinastahili kuwa wanachama kwa wakati mmoja, lakini maombi yao kuwa wanachama yanastahili kukubaliwa haraka iwezekanavyo.
Çavuşoğlu amesema kwamba Uturuki huenda ikatathmini maombi hayo lakini sio kwa pamoja.
Uturuki na Hungary ndio nchi pekee wanachama wa NATO ambazo hazijarasmisha uanachama wa Finland na Sweden kwenye muungano huo.
Finland na Sweden ziliomba kuwa wanachama wa NATO baada ya Russia kuivamia Ukraine, mwaka uliopita.
Uturuki imesita kuunga mkono ombi la Sweden, ikiishutumu serikali ya Sweden kwa kuwapatia hifadhi wanachama wa makundi ambayo Uturuki inatambua kwamba ni ya kigaidi.
Facebook Forum