Erdogan mwenye umri wa miaka 69, ameiongoza Uturuki kwa muda wa miaka 20, alishindwa kupata ushindi wa moja kwa moja katika duru ya kwanza ya uchaguzi mapema mwezi huu.
Kemal Kilicdaroglu, mwenye umri wa miaka 79 ndiye mshindani pekee wa Erdogan.
Uturuki inakabiliwa na matatizo makubwa ya kiuchumi, mfumuko wa bei na athari za tetemeko baya la ardhi lililotokea miezi mitatu iliyopita.
Ushindi wa Erdogan utamuwezesha kuwa kiongozi wa Uturuki kwa mwongo wa tatu.
Wakosoaji wake wanasema kwamba utawala wake umekuwa wa kidikteta.
Ukusanyaji wa maoni unaonyesha kwamba Erdogan ataibuka mshindi. Matokeo rasmi yanatarajiwa katika saa chache zijazo.
Forum