Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 17:26

Uteuzi wa Rex Tillerson bado unakabiliwa na pingamizi


Waziri mteule wa Mambo ya Nje wa Marekani, Rex Tillerson
Waziri mteule wa Mambo ya Nje wa Marekani, Rex Tillerson

Kamati ya Mambo ya Nje katika baraza la Seneti inategemea kupiga kura Jumatatu kuthibitisha chaguo la rais Donald Trump katika nafasi wa waziri wa mambo ya nje, ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya mafuta, Rex Tillerson.

Hata hivyo bado haijaeleweka iwapo Seneta wa Republikan, Marco Rubio atakubaliana na uteuzi huo.

Jumapili warepublikan wawili, Seneta John McCain na Lindsey Graham waliotoa ushirikiano wao kwa kumkubali Tillerson baada ya kuwa na kero kubwa kuhusu uhusiano wake na Russia.

Japokuwa bado tunayo manung’uniko kuhusu mahusiano yake na rais wa Russia, Vladimir Putin, tunaamini kuwa Bwana Tillerson anaweza kusimamia maslahi ya Marekani, “McCain na Graham wamesema katika mkutano na waandishi wa habari.

“Hii ilikuwa sio kazi nyepesi,” McCain amesema wakati akizungumza na shirika la habari la ABC, katika kipindi cha 'This Week'. Lakini bado naamini kunapokuwa na mashaka yoyote na rais aliyeingia madarakani lazima tuwe na hisia chanya juu yake.

Wakati kukubalika kwa mteule huyo na McCain na Graham kunampa nafasi Tillerson kupata nafasi hiyo, hakuna kati yao atayepiga kura katika kamati ya Seneti ya mambo ya nje ambayo itafanya maamuzi kuhusu uteule huo Jumatatu jioni.

Seneta warepublikan wa Florida, Rubio yuko katika kamati hii, lakini mpaka sasa bado hajatangaza iwapo atampitisha Tillerson.

Warepublikan wana nafasi moja katika kamati hiyo, na Tillerson atashindwa kupita kama Rubio akiungana na wademokrat ambao wanategemewa kupiga kura dhidi ya mkurugenzi huyo wa mafuta.

Wakati Seneta Tillerson akihojiwa kwa ajili ya kuthibitishwa, Rubio alimpa changamoto kuwa amwite Putin ni mhalifu wa kivita kwa sababu ya vitendo vya majeshi ya Russia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria.

Saa kadhaa baada ya Donald Trump kuapishwa kuchukua madaraka Ijumaa, Seneti iliwapitisha kwa pamoja wateule wake wanao ongoza Pentagon na Wizara ya Mambo ya Ndani. Lakini mpaka sasa wateule wengine wa Trump bado wanaonekana kuwa na utata.

Katika ukumbi wa Seneti wiki hii, warepublikani wameendelea kushinikiza kupitishwa kwa mteule katika nafasi ya mkurugenzi wa CIA, Mike Pompeo, ambaye kushindwa kwake kupitishwa Ijumaa kuliukasirisha uongozi mpya wa Trump White House.

Wademokrat hawawezi kuzuia uteuzi wa baraza lake Trump wao wenyewe na rais amesema ana imani kwamba timu yake itaingia kazini.

Nakumbuka vizuri kuwa Januari 2009, Seneti katika siku ya kwanza ya kuapishwa rais walipitisha mawaziri saba. Saba, na wala sio wawili,” alilalamika McCain.

“Kwa nini tusiende mbele na kumpa rais timu yake ya ulinzi wakati tunaihitaji kuliko wakati wowote katika historia ya nchi yetu,?"

Lakini wademokrat wanalalamika wateule wa Trump wamekuwa wakisusa kutoa maelezo ya mali zao na mambo yanayo husiana na maadili ya nyadhifa zao mpya.

XS
SM
MD
LG