Wakihukumiwa kifo katika kesi zilizofanyika kwa siri mwezi Januari na mwezi Aprili, wanaume hao walishtumiwa kulisaidia vuguvugu la kiraia la kupinga utawala wa kijeshi tangu mapinduzi ya kijeshi ya mwaka jana na ukandamizaji mbaya wa maandamano yaliyofanyika nchi nzima.
Miongoni mwa walionyongwa ni mtetezi wa demokrasia Kyaw Min Yu, anayejulikana kwa jina la Jimmy, na mbunge wa zamani na msani wa nyimbo za Hip-hop Phyo Zeya Thaw, mshirika wa kiongozi aliyeondolewa madarakani Aung San Suu Kyi.
Wengine walionyongwa ni Hla Aung na Aung Thura Zaw.
Mkuu wa Baraza la haki za binadamu la Umoja wa mataifa Michelle Bachelet amezitaja adhabu hizo za kunyongwa kuwa “hatua ya kikatili na ya kurudi nyuma” ambayo itaongeza tu kujiingiza kwake katika mzozo ambao nchi hiyo iliuanzisha yenyewe.
Marekani imelaani kitendo hicho na kusema kwamba hakutakuwa tena “ushirikiano wa kawaida” na uongozi wa kijeshi wa Myanmar.