Hii ikiwa hatua ya hivi karibuni katika mazungumzo na jumuiya ya kikanda ya ECOWAS kuondoa vikwazo vinavyodumaza uchumi.
Viongozi wa kijeshi wa nchi hiyo ya Afrika Magharibi wamekuwa chini ya shinikizo la kurejesha demokrasia tangu walipopindua serikali na kushindwa kutimiza ahadi ya kuandaa uchaguzi mwezi Februari, na kusababisha vikwazo kutoka Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS).
Muda wa mpito umewekwa kuwa miezi 24, msemaji wa serikali ya mpito Abdoulaye Maiga alisema kwenye televisheni ya kitaifa, na tarehe ya kuanza ikiwa Machi 26, 2022.