Utawala wa Biden unaliomba Bunge la Marekani kutoa zaidi ya dola bilioni 13 za msaada wa dharura wa ulinzi kwa Ukraine na dola bilioni 8 za ziada kwa msaada wa kibinadamu hadi mwisho wa mwaka.
Huu ni uingizwaji mwingine mkubwa wa fedha wakati uvamizi wa Russia unaendelea na Ukraine inasukuma shambulio la kulipiza kisasi dhidi ya vikosi vya Kremlin vilivyoingia kwa kiasi kikubwa.
Ombi la msaada huo pia linajumuisha dola bilioni 12 za kusaidia katika kurejesha fedha za maafa ya serikali kuu ya Marekani baada ya msimu mbaya wa hali ya hewa ya joto na dhoruba na fedha za kuimarisha utekelezaji wa majukumu katika mpaka wa Kusini na Mexico.
Forum