Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 06, 2024 Local time: 04:10

Utawala wa Biden kuongeza misaada Ukraine


Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken (kulia) alipokutana na Waziri wa Mambo ya nje wa Ukraine Andrii Sybiha (kushoto) huko Brussels November 13, 2024. picha na REUTERS
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken (kulia) alipokutana na Waziri wa Mambo ya nje wa Ukraine Andrii Sybiha (kushoto) huko Brussels November 13, 2024. picha na REUTERS

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken ameihakikishia NATO Jumatano kwamba, utawala wa Biden utaongeza misaada kwa ajili ya Ukraine katika miezi michache kabla Donald Trump kurejea kama rais wa Marekani na utajaribu kuimarisha umoja huo.

Akikutana na katibu mkuu wa NATO Mark Rutte mjini Brussels, Blinken pia alisema kupelekwa vikosi vya Korea Kaskazini kwa ajili ya kuisaidia Russia katika vita vya Ukraine kutopata jibu thabiti.

Blinken aliwaambia waandishi wa habari kuwa uhusiano wa Moscow na Pyongyang “ulikuwa wa pande mbili” na kuna wasiwasi mkubwa kuhusu kile ambacho Russia inafanya au inaweza kufanya ili kuimarisha uwezo wa Korea Kaskazini ikiwa ni pamoja na uwezo wake wa nyuklia.

Rais mteule Donald Trump ambaye aliwahi kuhoji msaada wa kijeshi wa Marekani kwa Ukraine, alisema atamaliza haraka vita vya Russia bila kueleza zaidi, ambapo ilizusha wasiwasi miongoni mwa washirika wa Marekani kwamba atajaribu kuilazimisha Kyiv kukubali amani kwa masharti ya Moscow.

Biden anaondoka madarakani Januari 20.

Forum

XS
SM
MD
LG