Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Septemba 18, 2024 Local time: 11:17

Utapia mlo waripotiwa Ethiopia


Wakimbizi katika eneo la Dollo Ado , Ethiopia.
Wakimbizi katika eneo la Dollo Ado , Ethiopia.

Idara ya UNHCR inasema utafiti juu ya hali ya watoto na lishe wanayopata katika kambi za Kobe na Hilaweyn unaonyesha kuwa watoto wa wakimbizi wa kisomali wako katika hali mbaya

Idara ya wakimbizi ya Umoja wa Mataifa inaripoti kiwango kikubwa cha utapia mlo miongoni mwa watoto wachanga katika kambi za Dollo Ado nchini Ethiopia. Kambi hizo pia ni makazi ya maelfu ya wakimbizi kutoka Somalia. Idara ya UNHCR inasema utafiti juu ya hali ya watoto na lishe wanayopata katika kambi za Kobe na Hilaweyn unaonyesha kuwa watoto wa wakimbizi wa kisomali wenye umri chini ya miaka mitano wako katika hali mbaya. Ufuatiliaji wa jamii ya kimataifa juu ya mzozo katika Pembe ya Afrika unaonekana kupamba moto. Lakini kulingana na Umoja wa Mataifa, mzozo huo bado unaendelea kushika kasi. Shirika hilo linasema zaidi ya watu milioni 12 wanaendelea kuathirika kutokana na mzozo mbaya wa ukame kuwahi kuathiri eneo hilo katika kipindi cha miaka 60. Watu wa Somalia ndiyo walioathirika zaidi kutokana na mzozo wa njaa na ukame.Msemaji wa UNHCR Andrej Mahecic aliambia sauti ya America kwamba idadi ya wasomali wanaotafuta hifadhi huko Ethiopia na Kenya imepungua hivi karibuni. Lakini anasema hali hiyo inasababishwa na vita na mvua kubwa inayonyesha huko Somalia kusini, hali ambayo inafanya usafiri kuwa wa shida.Anasema hata hivyo takriban watu 170 hadi mia 2 wanawasili kote Kenya na Ethiopia kila siku. Wengi wao wakitafuta chakula kwa ajili yao na wanao walioathirika mno na utapia mlo.

XS
SM
MD
LG