Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 02:55

UTANGULIZI-Uchaguzi Mkuu Kenya (2017)


Bendera ya Kenya
Bendera ya Kenya

Kenya wanafanya uchaguzi mkuu Agosti 8, 2017. Hivi sasa vyama vya siasa ambavyo vinashiriki katika uchaguzi viko katika kampeni kali za kunadi sera zao ili kuvutia wapiga kura wengi zaidi.

IEBC

Kwa Mujibu wa utaratibu ulioandaliwa na Tume ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) Kenya, uchaguzi utahusisha nafasi ya rais na makamu wake, wabunge, na viongozi wa serikali za mitaa.

Uchaguzi mkuu nchini Kenya hufanyika baada ya kila miaka mitano. Licha ya nchi hiyo kuwa imefanya chaguzi nyingi tangu 1962, bado kuna changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na ukabila na mizozo ya kisiasa. Mfano mmojawapo ni machafuko ya kisiasa yaliyotokea katika uchaguzi wa urais mwaka 2007/08.

Wanasiasa Wanane Wajitokeza Kugombea Urais

Katika kinyang’anyiro cha urais kuna wanasiasa wanane wanaowania nafasi hiyo. Rais aliyepo madarakani Uhuru Kenyatta na kiongozi wa upinzani Raila Odinga ni miongoni mwao. Pia kuna wagombea wagombea huru (hawana vyama).

Wengine waliopo katika mbio hizo za kuwania nafasi ya urais ni pamoja na Abduba Dida, anawania urais kupitia chama cha Alliance for Real Change (ARK) na muungano wa Tunza Coalition, Cyrus Jirongo anawania kupitia chama cha United Democratic Party (UDP). Wengine ni Ekuru Aukot kupitia chama cha Thirdway Alliance Kenya (TAK), Japhet Kaluyu (mgombea huru), Joseph Nyagah (mgombea huru), na Profesa Michael Wainaina (mgombea huru).

XS
SM
MD
LG