Utafiti huo uliochapishwa Alhamisi, ulifanya makadirio hayo baada ya kukagua kesi 2,225 za dhulma ya kingono zilizochunguzwa na kubaini wahusika 1,259 tangu mwaka wa 1946.
Idadi ndogo ya faili zilizotolewa na makanisa ya maeneo tofauti ya Ujerumani ilimaanisha kuwa huwenda idadi hiyo ilikuwa “tonya la maji katika bahari”, mchapishaji mwenza wa utafiti huo Martin Wazlawik amesema katika mkutano na waandishi wa habari.
Jumla ya makadirio ya idadi ya wahusika wa vitendo hivyo ilikuwa karibu 3,500 kati ya wachungaji na maafisa wa kanisa hilo, kulingana na utafiti ulioidhinishwa na kanisa la EKD.
Forum