Haya ni kulingana na utafiti uliofanywa na shirika la kukusanya maoni la Ipsos kwa ushirikiano na shirika la habari la Reuters.
Ukusanyaji huo wa maoni imefanyika wakati Marekani inakaribia kuchukua hatua za kuzia kabisa mtandao wa Tik Tok nchini Marekani.
Asilimia 58 ya waliohojiwa katika utafiti huo wa siku mbili wamesema kwamba China inatumia Tik Tok kushawishi fikra za Wamarekani.
Wamarekani Warepublican wanaamini sana kwamba China inatumia Tik Tok kuwashawishi Wamarekani, ikilinganishwa na Wademokrat.
Tik Tok imesema kwamba imetumia zaidi ya dola bilioni 1.5 kuimarisha usalama wa mtandao huo na kwamba haitatoa taarifa kuhusu watumiaji milioni 170 walio Marekani kwa serikali ya China.
Forum