Uswizi imesema Jumatatu kutakuwa na nchi takriban 90 na mashirika yatakayohudhuria mkutano wa siku mbili wa amani kuhusu Ukraine ambapo Uswizi ni mwenyeji wa mkutano huo kuanzia Jumamosi.
Serikali ya Uswizi imesema karibu nusu ya nchi hizo zinatoka Ulaya na kwamba ushiriki mpana wa kimataifa ni muhimu katika kuanzisha mchakato wenye msaada mkubwa.
Taarifa ya serikali imesema mkutano huo wa amani unalenga kuwa jukwaa la kujadili njia za kufanikisha amani ya pamoja, yenye haki, na ya kudumu kwa Ukraine kwa kuzingatia sheria za kimataifa na mkataba wa Umoja wa Mataifa, pamoja na kuw na muundo wa kutekeleza mpango wa amani na namna ya kuihusisha Russia na Ukraine katika mchakato wa amani. Uswizi ni mwenyeji wa mkutano huo kufuatia ombi la Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy, lakini Russia haishiriki.
Russia imekosoa mchakato huo na kusema itashiriki katika mazungumzo ya amani ikiwa tu watazingatia hali ilivyo nchini humo, ikijumuisha mafanikio ya Russia katika mapmbano tangu ilipoanzisha uvamizi wake kwa Ukraine hapo Februari 2022.
Forum