Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 14, 2024 Local time: 17:45

Sitisho la mapigano Syria bado linatekelezwa


Mtoto wa kiume raia wa Syria akisubiri basi katika mji wa Palmyra katika jimbo la kati ya Homs nchini Syria.
Mtoto wa kiume raia wa Syria akisubiri basi katika mji wa Palmyra katika jimbo la kati ya Homs nchini Syria.

Marekani inaamini miezi miwili ya usitishaji mapigano nchini Syria bado ipo na inatekelezwa licha ya kuongezeka kwa ghasia na shutuma za ukiukaji unaofanywa na waasi na serikali.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani, John Kirby, alisema jana Jumanne kwamba kiwango cha mapambano kipo chini kama ilivyokuwa kabla ya sitisho la mapigano kuanza kufanya kazi mwishoni mwa mwezi Februari.

Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa kwa Syria, Staffan de Mistura, alielezea ongezeko la ghasia ni jambo lenye kutia wasi wasi katika tathmini yake ya aribuni, lakini alisema pia kwamba usitishaji mapigano unafanyika katika maeneo mengi.

XS
SM
MD
LG