Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 12:43

Pakistan zakubaliana kusitisha mapigano Afghanistan


Mpaka wa Afghanistan and Pakistan, eneo la Torkham
Mpaka wa Afghanistan and Pakistan, eneo la Torkham

Pakistan na Afghanistan wamekubaliana kuhusu usitishaji wa mapigano leo Jumatatu baada ya mapigano madogo ya usiku kucha yaliyotokea kwenye mpaka, ambapo mtu mmoja aliuwawa na 18 wengine walijeruhiwa.

Maafisa na wakazi hata hivyo wanasema hali kwenye eneo la mpaka wa Torkham bado ni tete na mzozo umelazimisha familia zipatazo 200 za wapakistan kuhama makazi kwenda kwenye maeneo yaliyo salama.

Pakistan inataka kujenga uzio mpya na vikosi vya mpakani vya Afghanistan havikuruhusu hilo.

"Pakistan iliingia katika eneo hilo na kufyatua risasi kwa vikosi vya Afghanistan," mkurugenzi mkuu Abdullah Abdulah aliuambia mkutano wa mawaziri mjini Kabul. Alithibitisha kwamba majibizano ya ufyatuaji risasi ambayo yalidumu kwa saa saba, yalisababisha kifo cha mwanajeshi mmoja wa Afghanistan na sita wengine kujeruhiwa.

Upande wa Pakistan pia ulishuhudia vifo kwenye mapambano ya kuvuka mpaka wa Torkham.

XS
SM
MD
LG