Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 13, 2024 Local time: 22:56

Kerry azungumzia kuanza tena kwa sitisho la mapigano nchini Syria


Watu wakitembea kwenye vifusi vya majengo yaliyoharibiwa na shambulizi la anga kaskazini kwa Syria.
Watu wakitembea kwenye vifusi vya majengo yaliyoharibiwa na shambulizi la anga kaskazini kwa Syria.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry, amesema anakaribia kufikia maelewano ya kuanza tena kwa sitisho la mapigano nchini Syria ambalo litajumuisha mji mkubwa wa Aleppo ambako idadi ya waliopoteza maisha kutokana na mashambulizi ya anga imeendelea kuongezeka Jumatatu.

Kerry alikutana na mwenzake wa Saudia Arabia, mjini Geneva, mapema leo Jumatatu katika juhhudi za kuokoa mpango wa sitisho la mapigano uliosimamiwa na Marekani na Russia ambao karibu uvunjike wakati majeshi ya Syria yalipofanya mashambulizi ya anga huko Aleppo kwa na kusababisha majeruhi wengi raia.

Maafisa wa Marekani wanasema ushirikiano wa Russia ni muhimu katika kumaliza ghasia na changamoto kubwa ya Kerry ni kupata nia ya dhati kutoka Moscow ili kuiwezesha serikali ya Syria kuacha kushambulia Aleppo.

XS
SM
MD
LG