Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 08, 2024 Local time: 23:13

Ushiriki wa wanawake katika siasa za Kenya


Wanawake nchini Kenya wakichota maji kwenye tenki katika mtaa wa Mukuru Kwa Njenga, Nairobi, Kenya. March 10, 2022
Wanawake nchini Kenya wakichota maji kwenye tenki katika mtaa wa Mukuru Kwa Njenga, Nairobi, Kenya. March 10, 2022

Katika uchaguzi wa mwaka huu nchini kenya wanawake wanaonekana kuteuliwa au kujitokeza kuwania nafasi za uongozi ikiwemo wagombea wenza, wabunge na wawakilishi maalumu katika majimbo.

Wanawake wanachangia asilimia 23 ya viti vya bunge la taifa na seneti idadi ambayo inajumuisha viti vilivyotengwa kwa ajili ya wawakilishi wanawake pekee.

Wakati wanawake wengi wanashawishiwa kugombea nafasi hizo katika uchaguzi mkuu bado haiko bayana kama idadi yao itafikia theluthi mbili ya wanawake katika bunge na nafasi nyingine inavyoelezewa kikatiba.

Hamisa zaja ni mwanamke anayewania nafasi ya uwakilishi bungeni kupitia chama cha United green movement, Mombasa Kenya, anasema hadi sasa hakuna takwimu rasmi kuhusu husu ushiriki wa wanawake katika uongozi na uchaguzi mkuu nchini kenya, wanawake bado hawana uwakilishi wa kutosha na katika viwango vyote vya kufanya maamuzi.

Vyama vya kisiasa vimetoa ahadi nyingi kwa wanawake

Hata hivyo vyama mbalimbali vya siasa na ushirikiano wake vimejitokeza kuelezea kushughulikia masuala yanayohusu wanawake.

Hata hivyo takwimu zinaonyesha kuwa katika uchaguzi wa mwaka 2017 wanawake walikuwa asilimia 7.9 ya wabunge waliochaguliwa kutoka maeneo bunge 290, asilimia 6.4 ya magavana na maseneta asilimia 6.6 ya MCAs waliochaguliwa.

Ni Dhahiri kuwa wanawake waliojitokeza kuwania nafasi za uongozi wa kisiasa ni wengi , lakiji je watapita ? hilo ni jambo ambalo bado linasubiriwa kwa hamu kubwa.

Wanawake Kenya wana viti vyao maalum bungeni

Grace Oloo ni mchambuzi wa masuala ya kisiasa nchini kenya anazungumzia uwakilishi wa nafasi za wagombea wanawake nchini Kenya kulinga na katiba ya nchi inayopendekeza kuwepo na theluthi mbili ya nafasi za wanawake katika uongozi wa kisiasa, changamoto gani hasa zinajitokeza kwa upande wa kundi hili la wanawake?

Macho na masikio yameelekezwa kuona ni umbali gani wanawake wanaowania nafasi za uongozi nchini humo watafikia. Wachambuzi wa mambo wanasema mwaka huu wa uchaguzi umevunja rekodi kwa wagombea uraisi walio mstari wa mbele kuwachagua wagombea wenza wanawake. Wengine wanajiuliza je ni ushindani wa kisiasa au ni wakati umefika wa wanawake kujitokeza na kumudu katika nafasi kubwa za kuongoza nchi?

Kujibu hilo Mchambuzi Grace Oloo anaeleza mtazamo wake kuhusu ushindani wa kisiasa uliopo Kenya kwa sasa.

Mbona wanawake wachache wanawania nafasi za uongozi Kenya?

Kumekuwa na sababu mbalimbali zilizopelekea uwakilishi mdogo wa wanawake katika uongozi wa kisiasa kenya. Mojawapo ni matokeo ya athari kwa mila na tamaduni ambazo zimepitwa na wakati na hilo linajionyesha katika mchango wa jinsia katika jamii . Baadhi ya wanawake nchini kenya wanaona mila na tamaduni zinaanza pole pole kuachwa kando na wanawake wanasonga mbele .

Mwanasheria wa katiba Bobby Mkangi anaeleza kama makubaliano ya kisheria na katiba yanafikiwa wakati huu kuhakikisha usawa katika uongozi wa kisiasa.

Hadi sasa wanawake walioteuliwa kuwa wagombea wenza walioko mstari wa mbele e wa kiti cha urais ni Martha Karua kupitia chama cha Azimio la umoja, Justina Wamae chama cha Roots na Ruth Mutua wa chama cha Agano.

XS
SM
MD
LG