Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 25, 2024 Local time: 22:18

Usalama wazidi kuharibika Burundi


Wakazi wa Bujumbura wakitafuta hifadhi kutokana na ukosefu wa usalama
Wakazi wa Bujumbura wakitafuta hifadhi kutokana na ukosefu wa usalama

Mashambulizi kadhaa yametokea katika mji mkuu wa Burundi, Bujumbura na kujeruhi polisi wanne.

Mashambulizi kadhaa yametokea katika mji mkuu wa Burundi, Bujumbura na kujeruhi polisi wanne. Mashambulizi matatu yalitokea mjini humo Jumatatu asubuhi katika mitaa mitatu ya Bujumbura wakati mengine yalifanyika usiku wa kuamkia Jumatatu. Milio ya risasi ilisikika Jumapili usiku katika mitaa ya Bwiza, katikati ya Bujumbura, wakati moja ya maguruneti ya Jumatatu asubuhi lilipiga katika eneo la Buyenzi lakini hakukuwa na madhara yoyote.

Riporti kuhusu usalama Bujumbura
please wait

No media source currently available

0:00 0:02:19 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Makazi ya meya wa jiji la Bujumbura ni miongoni mwa sehemu zilizolengwa lakini Meya hakudhurika. Hali ya usalama Burundi imezidi kuzorota katika siku za hivi karibuni kutokana na ghasia zilizoanzia pale Rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza kutangazwa na chama chake kuwa mgombea urais kwa mara ya tatu na hatimaye kuchaguliwa katika uchaguzi mkuu uliofuatiwa na ambao ulisusiwa na vyama vya upinzani.

Mwishoni mwa wiki iliyopita Rais Barack Obama wa Marekani alituma ujumbe wa video kwa watu wa Burundi kuwataka kuishinikiza serikali yake kufanya mazungumzo na makundi mbali mbali nje ya nchi hiyo kutafuta amani ya kudumu. Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa pamoja na Umoja wa Afrika pia zimeshinikiza serikali ya Burundi kufanya mazungumzo na makundi yanayopinga serikali kutafuta suluhisho la amani.

XS
SM
MD
LG