Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 03:30

Obama ahimiza usalama wa chakula barani Afrika


Rais wa Marekani, Barack Obama ni mwenyeji wa mkutano wa G8 unaofanyika Washington DC
Rais wa Marekani, Barack Obama ni mwenyeji wa mkutano wa G8 unaofanyika Washington DC

Chakula cha asilimia 80 ya nchi zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara barani Afrika kinazalishwa na wakulima wadogo wadogo

Rais wa Marekani Barack Obama anahimiza usalama wa chakula barani Afrika Ijumaa huko Washington nchini Marekani na atalizungumzia zaidi suala hilo kwenye mkutano unaofuata wa G8.

Rais Obama anatazamiwa kuzungumza na viongozi wa bara la Afrika kwenye mkutano unaofanyika Ijumaa juu ya usalama wa chakula. Juhudi mpya za mkutano wa Ijumaa zinatarajiwa kulenga watu milioni 50 wasio na chakula kwa kuongeza uwekezaji wa kilimo.

Katika nchi zilizo chini ya jangwa la Sahara barani Afrika takribani asilimia 80 ya chakula bado kinazalishwa na wakulima wenye uwezo mdogo. Suala hilo pia lipo kwenye ajenda ya mkutano wa G8 unaofanyika mjini Washington.

Rais Obama amemualika Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete,Waziri Mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi, Rais wa Ghana John Atta Mills na Rais wa Benin Boni Yayi kuhudhuria mkutano huu wa G8 utakaofanyika Camp David eneo lililotengwa kwa mapumziko ya marais wa Marekani, nje kidogo ya jiji la Washington DC.

XS
SM
MD
LG