Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 19:00

Uganda yapiga marufuku usafirishaji ndege kudhibiti mafua ya ndege


Uganda yachukua tahadhari kudhibiti mafua ya ndege.
Uganda yachukua tahadhari kudhibiti mafua ya ndege.

Serikali ya Uganda imepiga marufuku usafirishaji ndege kutoka maeneo ambayo yamekumbwa na mafua ya ndege, ikiwa ni tahadhari iliyochukuliwa kuzuia ugonjwa huo kusambaa maeneo mengine.

Mwandishi wa Idhaa ya Kiswahili ya VOA, Kennes Bwire amesema serikali imetangaza karantini hiyo wakati harakati za utafiti zikiendelea.

Hata hivyo wizara ya kilimo Jumapili ilithibitisha kuwepo kwa mafua ya ndege aina ya HPA1 baada ya kufanya uchunguzi wa ndege waliokutwa wamekufa katika ufukwe wa ziwa Victoria kwenye eneo kati ya Kampala na Entebbe, ambako uko uwanja wa ndege.

Ndege walikutwa pia wamekufa katika wilaya ya Nasaka. Vipimo hivyo vimeonyesha kuwepo kwa mafua ya ndege,

Wizara ya Kilimo imethibitisha hilo katika mkutano wake na waandishi wa habari Jumapili.

Waziri wa Kilimo katika ofisi ya rais, Kibazanga Christopher amesema ndege hao wanashukiwa kuwa wametokea Ulaya, na ameagiza nchi zote jirani kuanza mara moja kuchukua hatua za kuwatahadharisha wananchi wao na kufuatilia kwa karibu makundi ya ndege yanayohamia katika maeneo yao kuchunguza kama ugonjwa huo umeenea huko.

Lutembe Bau, ni eneo kubwa linalopokea ndege wanaofanya safari zao wakiwa njiani kurejea Afrika au kuondoka kwenda UIaya na ni moja ya maeneo ambayo ndege hao walikutwa wamekufa.

Kuzuka kwa mafua ya Avian nchini Uganda ni habari mbaya kwa wasafiri na utalii kwa nchi za Afrika Mashariki .

Kwa mujibu wa tovuti ya Shirika la Afya Duniani (WHO), mafua ya ndege au "avian" ni ugonjwa unaoambukizwa na ndege. Kwa kirusi hicho cha avian kawaida sio chenye kumuambukiza mwanadamu lakini imewahi kusababisha matatizo ya kupumua kwa wanadamu.

Homa kali ya mafua ya ndege inapomshambulia ndege, uwezekano wa kufa ni asilimia 100. Hivyo, homa kali ya mafua ya ndege inachukuliwa na Shirika la Afyakuwa ni maradhi hatari ya wanyama ya ngazi A.

Hata hivyo hii ni mara ya kwanza mafua ya ndege kuthibitishwa kuwepo Afrika Mashariki.

Nigeria, Cameroon, Afrika ya Kati na Afrika Kusini zimewahi kutoa taarifa za mafua ya ndege katikati ya mwaka 2016.

XS
SM
MD
LG