Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 17, 2024 Local time: 14:32

Suala la Brexit latawala siasa Marekani


Wagombea urais mwaka 2016 Marekani Donald Trump na Hillary Clinton
Wagombea urais mwaka 2016 Marekani Donald Trump na Hillary Clinton

Uwamuzi wa Uingereza kuondoka katika umoja wa ulaya ni mada iliyotawala katika mbio za uchaguzi wa rais Marekani.Mgombea mtarajiwa kutoka chama cha Republican Donald Trump anaona hatua ya Uingereza kama thibitisho kwa ujumbe msingi wa kampeni yake. Wakati huohuo mgombea Hillary Clinton anaona matukio hayo kama ushahidi zaidi kuwa Trump hafai kuwa rais.

Ushindi wa Uingereza kujitoa katika umoja wa Ulaya umesababisha utawala wa Obama kutoweka sura nzuri katika matokeo ambayo haukutaka.

Waziri Kerry alisema kuwa,taifa moja limefanya uwamuzi. Bila shaka ni uwamuzi ambao Marekani ulitarajia utakwenda upande mwengine, lakini hilo halikutokea. Kwa hivyo tunaanza kwa kuwa na heshima kubwa kwa wapiga kura.

Lakini mgombea wa chama cha Republican Dobald Trump alionekana kuuikaribisha uwamuzi huo.

Trump alisema kuwa watu wanataka kumiliki tena taifa lao. Wanataka kuwa huru, nnaona usawa baina ya kile kinachofanyinka Marekani na kinachofanyika huko. Watu wanataka kudhibiti mipaka yao.

Naye mgombea mtrajiwa wa chama cha democratic Hillary Clinton, akosoa kauli ya Trump kuwa mzozo wa Uingereza huwenda ukanufaisha biashara zake huko Scotland

Lakini kura ya Uingereza ya kujitoa katika umoja wa ulaya ilimulika kutokuridhika kwa umma upande mmoja wa bahari ya Atlantic, na warepublican wanasema hisia kama hizo ziko upande huu wa Atlantic.

Seneta mrepublican Mitch Mcconell akizungumza katika kipindi cha This week kwenye televisheni ya ABC alisema.

Seneta McConell alisema, kile ulichokiona Uingereza kutokana na vile nilivyoelewa, ni kwamba watu wamechoshwa na viongozi ambao hawakuchaguliwa huko Brussels. Na bila shaka tuna hisia hizo hapa pia. Watendaji wengi serikalini wanapanua kanuni kwa njia ambazo zinadumazaa uchumi na kufanya ukuwaji kuwa mgumu.

Takwimu mpya ya maoni inaonyesha Bi Clinton akiongoza dhidi ya Trump, lakini wapiga kura wengi wanataka muelekeo mpya kwa Marekani. Wademokrat wanasisistiza kuwa wapiga kura hawajapotoshwa na kutokuridhika.

Waziri wa ajira Tom Perez, akizungumza kwenye kipindi cha This week katika televisheni ya ABC, anasema.

Naye Perez alisema,tofauti baina ya katibu Clinton a Donald Trump kwa mithili ya tabia, mithili ya kufanya hikma ni tofauti sana. Na zinadhihirika tena katika kipindi hiki cha wiki mbili zilopita.

Wimbi la tetemeko la kura ya kujitoa uingereza katika umoja wa ulaya limeshutusha uchumi wa marekani unaoibuka taratibu, huwenda ikawa ndio suala kuu katika uchaguzi ujao. Utawala wa Obama unasisitiza haja ya kupunguza michanganyo inayotokana na hatua ya uingereza.

XS
SM
MD
LG