Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 28, 2023 Local time: 22:19

Marekani na Uingereza zaingia raundi ya pili


Landon Donovan, kati, wa Marekani akisherehekea na wachezaji wenzake baada ya kufunga goli la ushindi dhidi ya Algeria katika uwanja wa Loftus Versfeld,Pretoria.

Marekani imefanikiwa kuingia raundi ya pili ya fainali za kombe la dunia baada ya ushindi mgumu wa 1-0 dhidi ya Algeria.

Marekani imefanikiwa kuingia raundi ya pili ya fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini baada ya kuishinda Algeria 1-0 katika mechi kali ya kundi C mjini Pretoria.

Baada ya kukosa nafasi chungu nzima mapema katika mechi hiyo, Landon Donovan aliachia mkwaju mkali kimiani katika dakika ya 91 na kuipa Marekani ushindi. Ushindi huo umewezesha Marekani kumaliza mechi za kundi ikiwa juu kwa pointi tano.

Uingereza pia ilifanikiwa kuingia raundi ya pili baada ya kuifunga Slovenia 1-0 kwa bao la Jermain Defoe katika dakika ya 23. Lakini Marekani inaoongoza kundi hilo kwa idadi ya magoli. Algeria na Slovenia wameyaaga mashindano hayo kutoka kundi C.

Ghana wamekuwa wawakilishi wa kwanza kwa Afrika kwenye michuano hii kuingia raundi ya pili ikiwa ni mara ya pili kwa nchi hiyo licha ya kupoteza mchezo dhidi ya Ujerumani kwahiyo hivi sasa watakutana na Marekani kwenye raundi ya pili.

Mechi hiyo itakuwa ni ya pekee kwani Marekani na Ghana wana historia ambapo Marekani itakuwa inatafuta kulipa kisasi baada ya kutolewa na Ghana kwenye mashindano yaliopita na pia kwenda robo fainali na si tu hivyo itakuwa mbele ya rais wao Barack Obama aliyeahidi kwenda kuwaona wakivuka raundi ya kwanza.

Ghana walikuwa na nafasi kdhaa za kufunga mabao lakini walizipoteza na walikuwa ni Australia wasiotegemewa kushinda kuifunga Serbia 2-1 waliowapa nafasi Ghana ya kusonga mbele.

Australia waliwashangaza waserbia kwa kuwachapa mabao 2-1na wamemaliza wakiwa na pointi 4 sawa na Ghana lakini wamefungwa magoli mengi zaidi kuliko Ghana na hilo limesababisha wao kuaga mashindano hayo.

XS
SM
MD
LG