Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 10, 2023 Local time: 16:57

Obama awasilisha mpango wa kuwasambaratisha LRA


Kiongozi wa LRA, Joseph Kony, (L)
Kiongozi wa LRA, Joseph Kony, (L)

Rais wa Marekani Barack Obama amewasilisha bungeni mpango wa utawala wake wa kuunga mkono kulinyang’anya silaha kundi la Lord’s Resistance Army-LRA, nchini Uganda.

Rais wa Marekani Barack Obama amewasilisha bungeni mpango wa utawala wake wa kuunga mkono kulinyang’anya silaha kundi la Lord’s Resistance Army-LRA, nchini Uganda.

Katika barua yake kwa wabunge waandamizi hapo Jumatano, bwana Obama alisema mpango unatoa muundo kwa Marekani kuhusika katika juhudi za kuwalinda raia na kuondoa vitisho vinavyoletwa na kundi la uasi, ambalo limeongoza kampeni ya vifo na uharibifu kwa miongo miwili.

Mapema mwa mwaka huu, rais Obama alitia saini sheria iliyolenga kuisaidia Uganda na mataifa mengine ya Afrika kupambana na waasi na kuyakamata tena maeneo ya kaskazini mwa Uganda ambako kundi awali lilikuwa makao yake.

Kiongozi wa LRA, Joseph Kony anatafutwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu kwa madai ya uhalifu dhidi ya binadamu. Anahama hama kuepuka kukamatwa.

Ripoti ya karibuni ya kundi la kimataifa linaloshughulika na migogoro, International Crisis Group, lenye makao yake Brussels, linasema Kony huenda hivi sasa anafanyia shughuli zake magharibi mwa Sudan katika mkoa wa Darfur.

Mwezi August, Human Rights Watch lilisema LRA limeuwa zaidi ya watu 250 huko Jamhuri ya Afrika ya Kati na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo mwanzoni mwa mwaka. Kundi hilo lilisema waasi waliwateka nyara watu wengine 700 na kuwalazimisha kuwa wanajeshi au watumwa wa ngono.


XS
SM
MD
LG