Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Julai 23, 2024 Local time: 14:48

Wagombea wa Democrat wagawana ushindi wa jimbo


Wagombea wa urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Democratic seneta Bernie Sanders andwaziri wa zamani wa mambo ya nje Hillary Clinton.
Wagombea wa urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Democratic seneta Bernie Sanders andwaziri wa zamani wa mambo ya nje Hillary Clinton.

Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani, Hillary Clinton na mpinzani mwenzake wa chama cha democrat, seneta wa Vermont, Bernie Sanders wamegawana ushindi kwenye uchaguzi wa awali uliofanyika katika majimbo ya Kentucky na Oregon, na kupelekea Clinton kukaribia kupata idadi ya wajumbe wanaohitajika katika uteuzi wa chama katika muda wa wiki tatu.

Clinton alimshinda Sanders katika jimbo la Kentucky kwa kiasi cha kura 2000, ambapo maafisa wa uchaguzi walisema wasingeweza kumtangaza mshindi kamili kwa kuwa kura zilikaribiana mno, lakini Clinton alidai kupata ushindi ukiwa ni wa kwanza kwa mwezi huu wa Mei.

Wakati huo huo Sanders aliongoza katika jimbo la Oregon. Kufuatia matokeo kwenye majimbo hayo mawili, Clinton anawania kuwa rais wa kwanza mwanamke hapa nchini, kama anafika kwenye uteuzi hapo Juni 7, wakati majimbo sita yanapopiga kura. Wademokrat, kisha watamtangaza rasmi Clinton kwenye mkutano wao mkuu wa chama mwezi Julai.

XS
SM
MD
LG