Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 22:06

Marekani kuendelea kuisaidia NATO nchini Libya


Hillary Clinton, waziri wa mambo ya nje wa Marekani.
Hillary Clinton, waziri wa mambo ya nje wa Marekani.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton anasema Marekani itaendelea kusaidia shughuli za NATO nchini Libya hadi kazi yake inakamilika.

Akizungumza na mawaziri wa mambo ya nje wa NATO mjini Berlin, leo Alhamis, Clinton alisema ni muhimu kwa ushirika kuendeleza umoja wao wakati kiongozi wa Libya Moammar gadhafi anawajaribu.

Wanachama wa ushirika huo wamegawanyika iwapo wazidishe kampeni za mabomu dhidi ya majeshi yanayomtii kanali Gadhafi. Uingereza na Ufaransa wamewataka washirika kuwekeza zaidi katika operesheni ya kijeshi, wakati Marekani inataka kupunguza uwajibikaji wake katika oparesheni hiyo.

Waasi wanajitahidi kudhibiti miji michache ambayo wameweza kuiteka kutoka majeshi ya serikali. Leo Alhamisi, waasi wanasema majeshi ya bwana Gadhafi yalifyatua roketi ndani ya mji wa Misrata na kuwauwa watu wasiopungua tisa. Serikali imekuwa ikishutumiwa kuwalenga raia katika mji wa bandari.

Mkutano mwingine wa kimataifa juu ya Libya unafanyika kwenye makao makuu ya umoja wan chi za kiarabu -Arab Leaque mjini Cairo. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon na mkuu wa sera za mambo ya nje katika Umoja wa Ulaya, Catherine Ashton wanashiriki, kama ilivyo kwa wawakilishi wa Umoja wa Afrika na taasisi ya chi za ki-Islam-OIC.

XS
SM
MD
LG