Mchezaji Jawad Adekoya wa Kwara Falcons aliipatia timu yake uongozi wa mapema kwa kupachika pointi tatu kutoka kwenye kona ya uwanja.
Naye Ruot Monyyong mwenye urefu wa futi na nchi 11 wa Falcons anaongeza na dunki baada ya kuchukua pasi kutoka kwa Mordi.
Naye Jeremiah Mordi alipachika pointi tatu kutoka karibu na eneo la kurushia mpira wa adhabu na kuwaweka Falcons mbele katika nusu ya kota ya pili.
Na dakika zikisonga mbele Monastir walianza kubadilika na huku akielekea kwenye eneo la kufunga Oussama Marnaoui aliruka juu na kusogeza mpira kwa Mokhtar Ghazaya ambaye alimalizia na danki na kuwaweka Monastir karibu kwenye mchezo huo .
Katika dakika ya 46 Ibrahima Thomas aliruka na kupachika pointi lakini alifanyiwa madhambi na kukata uongozi wa Falcons kuelekea mwisho wa kota ya pili.
Katika dakika ya 54 Adekoya anajibu kwa pointi tatu kubwa kutoka eneo la mpira wa adhabu ili kufunga mchezo na mchezo kuwa sare katikati ya kota ya tatu.
Lakini mabingwa watetezi US Monastir walionyesha bado wamo na mshmbuliaji Marnaoui alipiga pointi tatu akiwa kwenye kona na kupunguza uongozi wa Falcons karibu na mwisho wa kota ya tatu.
Na vijana wa Monastir walichukua uongozi mapema katika kota ya nne na pointi tatu zilizowekwa nyavuni na Bouallegue.
Naye mchezaji mkongwe anayeweka rekodi Radhouane Slimane mwenye umri wa miaka 43 alianza na mpira na kupokea pasi kutoka kwa Firas Lahyani na kumalizia kwa dunki ambayo iliwatoa Falcons mchezoni.
Hatimaye Ibrahima Thomas anapiga pointi tatu muhimu katika sekunde za mwisho za mchezo huo, na kuwapa mabingwa watetezi ushindi wa jumla ya pointi 85-75.