Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 07:32

Marekani yapata mwanasheria mkuu mpya


Mwanasheria Mkuu mpya wa Marekani Loretta Lynch.
Mwanasheria Mkuu mpya wa Marekani Loretta Lynch.

Marekani leo imemwapisha Loretta Lynch kama Mwanasheria Mkuu mpya kuchukua nafasi ya Mwanasheria Mkuu aliyepita Eric Holder.

Makamu Rais Joe Biden aliongoza sherehe zilizofanyika katika Wizara ya Sheria. Lynch anaingia katika historia kama mwanamke wa kwanza Mmarekani mweusi kushika wadhifa huo.

Imechukua karibu miezi sita tangu Rais Obama kumteua Bi Lynch kuchukua nafasi hiyo, huku uteuzi wake ukipata upinzani mkubwa katika bunge la Marekani. Hatimaye, baraza la Seneti liliidhinisha uteuzi huo Alhamisi Aprili 23, 2015.

Lynch anamfuatia Holder ambaye naye alikuwa Mmarekani wa kwanza mweusi kushika wadhifa huo kabla ya kustaafu baada ya miaka sita.

Lynch anachukua wizara ya sheria ikiwa imebaki miaka miwili tu kabla ya kumalizika kwa utawala wa Rais Obama, na wakati ambapo mwenendo wa polisi nchini unafuatiliwa kwa karibu baada ya matukio kadha ya polisi kukabiliwa na madai ya kukikua hadi za raia.

XS
SM
MD
LG