Polisi wa Jamaica wanasema watu 73 wameuwawa tangu maafisa waanze mashambulizi kwa kiongozi anayeshutumiwa kwa uuzaji wa madawa ya kulevya anayetafutwa na Marekani.
Maafisa walitangaza kuongezeka kwa idadi ya waliokufa Alhamisi.
Kulipuka kwa ghasia hizo kulichangiwa na uamuzi wa serikali ya Jamaica kumpeleka nchini marekani Dudus Coke. Anatafutwa Marekani kwa shutuma za usafirishaji wa madawa ya kulevya na silaha.