Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Oktoba 07, 2022 Local time: 03:00

Mswaada wa Marekani kupambana na madini haramu DRC


Wanawake mashariki mwa DRC ni waathirika wakubwa wa mapigano yanayochochewa na mauzo ya madini haramu.

Mswaada wa mageuzi ya fedha uliotiwa saini na Rais Barack Obama utapambana pia na madini kutoka DRC yapatikanayo kwa njia haramu.

Mswaada wa mageuzi ya fedha uliotiwa saini na Rais Barack Obama mjini Washington Jumatano una kipengele chenye shabaha ya kupambana na biashara ya madini yanayotokana na migogoro mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Kipengela hicho ambacho kiliwekwa katika "mengineyo" kinayataka maelfu ya makampuni ya Marekani kueleza yanachukua hatua gani kuhakikisha kuwa bidhaa zao ikiwa ni pamoja na kompyuta aina ya laptops, simu za mkononi na vifaa vya tiba havitengenezwi kwa kutumia madini yanayojulikana kama "madini ya migogoro" kutoka DRC. Fedha zinazotokana na mauzo ya madini ya namna hii ndiyo yaliyodhamini karibu miaka 15 ya mapigano yaliyojaa vitendo vya unyanyasaji wa wanawake mashariki mwa DRC.

Ingawa swala hilo halikutajwa katika mjadala wa mswaada huo wa mageuzi ya fedha katika bunge la Marekani lakini limeungwa mkono na wabunge kutoka pande zote nchini Marekani na mpaka wanaharakati wanaopigania haki za binadamu duniani.

Kwa miaka kadha wanaharakati wamekuwa wakieleza kuwa madini ya mashariki mwa DRC ndio chanzo cha mapigano yasiyokwisha katika eneo hilo, na kusababisha mateso kwa wananchi hasa wanawake na wasichana wadogo ambayo wamekuwa wakikabiliana na vitendo vya ubakaji.

XS
SM
MD
LG