Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 05:01

Clinton apata ushindi mkubwa S. Carolina, aangazia macho 'Super Tuesday'


 Bi Hillary Clinton, siku ya Jumamosi  alimshinda kwa kiasi kikubwa cha kura mpinzani wake wa pekee katika chama chao cha Democratic Bernie Sanders kwenye uchaguzi wa mchujo wa urais katika jimbo la South Carolina
Bi Hillary Clinton, siku ya Jumamosi  alimshinda kwa kiasi kikubwa cha kura mpinzani wake wa pekee katika chama chao cha Democratic Bernie Sanders kwenye uchaguzi wa mchujo wa urais katika jimbo la South Carolina

Hillary Clinton, siku ya Jumamosi  alimshinda kwa kiasi kikubwa cha kura mpinzani wake wa pekee katika chama chao cha Democratic Bernie Sanders kwenye uchaguzi wa mchujo wa urais katika jimbo la South Carolina.

Na BMJ Muriithi

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton, siku ya Jumamosi alimshinda kwa kiasi kikubwa cha kura mpinzani wake wa pekee katika chama cha Democratic, Seneta wa jimbo la Vermont, Bernie Sanders, kwenye uchaguzi wa mchujo wa urais katika jimbo la South Carolina.

Bi Clinton alipata asilimia 73 ya kura huku Sanders akipata asili mia 23 katika jimbo hilo la pwani ya Mashariki mwa Marekani, ambalo lina wapiga kura wengi wa asili ya Kiafrika.

Akitoa hotuba yake Jumamosi usiku, Bi Clinton alisema ana matumaini makubwa kwamba atapata wajumbe wengi wa kuiunga mkono safari yake ya kujaribu kuingia ikulu ya White House kama rais kwenye uchaguzi muhimu zaidi utakaofanyika siku ya Jumanne ulio maarufu kama "Super Tuesday."

"Sasa kura hizi za awali zimeanza kuchukua mkondo wa kitaifa," alisema Bi Clinton huku wafuasi wake na mashabiki wakijibu kwa shangwe vigelegele na makofi.

Sanders alimpongeza Bi Clinton kwa ushindi katika hotuba aliyoitoa akiwa kwenye jimbo la Oklahoma. Hata hivyo, mwanasiasa huyo mkongwe alisema vita vya kumtafuta atakayepeperusha bendera ya chama cha Democratic bado vitaendelea. "Mambo bado," alisema Bw Sanders.

Awali, Clinton alikuwa ameshinda majimbo ya Iowa na Nevada huku Sanders akishinda katika jimbo la New Hampshire.

Clinton, mwenye umri wa miaka 68 anapigania tikiti ambayo alipigania tena miaka saba iliyopita aliposhindwa na rais wa sasa wa Marekani, Barack Obama. Uchaguzi wa mchunjo utakaofanyika Jumanne ni muhimu mno kwani msimamo wa wajumbe zaidi ya 1,000 kutoka majimbo zaidi ya kumi utajulikana siku hiyo huku mshindi akipata nafasi bora zaidi ya kushindania urais na yule atakayechaguliwa kwa upande wa Warepublikan.

Jumanne iliyopita, Donald Trump aliwashinda kwa asili mia kubwa wawaniaji wenzake kwa tikiti ya Republican katika jimbo hilo la South Carolina.

Sasa macho yote yanalenga siku ya "Super Tuesday" ambayo inatarajiwa kupeana mwelekeo dhahiri zaidi kwa siasa za urais wa Marekani za mwaka wa 2016.

XS
SM
MD
LG