Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 13:24

Marekani yapeleka wanajeshi Cameroon kupambana na Boko Haram

Wanajeshi wa Cameroon kwenye kijiji cha Mabass, wakilfanya ulinzi dhidi ya wanamgambo wa Boko Haram
Wanajeshi wa Cameroon kwenye kijiji cha Mabass, wakilfanya ulinzi dhidi ya wanamgambo wa Boko Haram

Rais Obama alitangaza kupelekwa kwa wanajeshi hao katika barua aliyowatumiwa wakuu wa baraza la senate na la wawakilishi. Anasema takriban wanajeshi 90 walianza kupelekwa huko Cameroon jumatatu, na idadi kamili ya wanajeshi wanaotazamiwa kupelekwa huko ni mia 3.

please wait

No media source currently available

0:00 0:01:10 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Rais Barack Obama atapeleka wanajeshi wa Marekani huko Cameroon kwa ajili ya upelezi wa angani dhidi ya wanamgambo wa Boko Haram. Afisa wa wizara ya ulinzi ya marekani amesema wanajeshi hao walialikwa na serikali ya Cameroon kama sehemu ya juhudi pana ya kimataifa kuzuia kuenea kwa wanamgambo wenye siasa kali huko Africa Magharibi

Afisa huyo wa Pentagon, anasema, haja ya Jumuia ya kimatiafa kuchukua hatua imezidi kuwa na umuhimu, pale Boko Haram na makundi mengine yanapoimarisha ghasia zao.

Boko Haram imekuwepo huko Kaskazini mwa Cameroon, ambayo iko karibu na mpaka na ngome ya kundi hilo huko kaskazini Mashariki mwa Nigeria. Kundi hilo limeuwa mamia ya raia huko Cameroon, na takriban raia elfu 10 nchini Nigeria katika miaka ilopita.

Rais Obama alitangaza kupelekwa kwa wanajeshi hao katika barua aliyowatumiwa wakuu wa baraza la senate na la wawakilishi. Anasema takriban wanajeshi 90 walianza kupelekwa huko Cameroon jumatatu, na idadi kamili ya wanajeshi wanaotazamiwa kupelekwa huko ni mia 3.

Msemaji wa wizara ya ulinzi, lutein kanali, Michelle Baldanza, alisema wanajeshi hao watasaidia kazi za kukusanya habari za kijasusi na upelelezi kwa ndege katika eneo hilo.

Kadhalika, kufuatana na maafisa wa ulinzi mbali na kuongoza ndege zisizokuwa na rubani wala silaha wanajeshi hao watazingatia katika kuwezesha operesheni, usalama wa mipaka na uwezo wa kikosi cha kujibu kwa haraka.

XS
SM
MD
LG