Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 08:42

Marekani yashambulia ngome ya Islamic State nchini Libya


US Islamic State
US Islamic State

Wizara ya ulinzi ya Marekani, ilitangaza siku ya Jumatatu kuwa jeshi lake limefanya mashambulizi ya anga huko Libya, ambayo yalilenga maeneo yanayoaminika kudhibitiwa na wanamgambo wa Islamic State.

Maafisa wa serikali ya Tripoli waliusema mashambulizi hayo yalilenga ngome ya Islamic State katika mji wa Sirte baada ya kuombwa na serikali ya umoja wa kitaifa ya nchi hiyo inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa, GNA. Pentagon ilisema kuwa rais Barack Obama aliidhinisha mashambulizi hayo, katika kuunga mkono vikosi vinavyoungana na GNA, baada ya kupokea pendekezo la waziri wa Ulinzi Ash Carter na mwenyekiti wa muungano wa wakuu wa kijeshi wa Marekani, Jenerali Joe Dunford.

Msemaji wa Pentagon Peter Cook anasema kombora moja liliharibu kifaru cha Islamic State kilichokua kinasababisha kitisho cha moja kwa moja dhidi ya wanajeshi wa serikali, na kuwashambulia raia kiholela.

XS
SM
MD
LG