Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 06:41

Jeshi la Marekani lafanya shambulizi mjini Kunduz, Afghanistan


Waziri wa ulinzi wa Marekani Ash Carter. Jeshi la Marekani lilifanya mashambulizi kwenye mji wa Kunduz, Kaskazioni mwa Afghanistan mapema Jumatano.
Waziri wa ulinzi wa Marekani Ash Carter. Jeshi la Marekani lilifanya mashambulizi kwenye mji wa Kunduz, Kaskazioni mwa Afghanistan mapema Jumatano.

Jeshi la Marekani lilisema mapema Jumatano kuwa lilifanya mashambulizi kwenye mji wa kaskazini mwa Afghanistan wa Kunduz katika juhudi za kulinda wanajeshi wa serikali wanaokabiliana na kundi sugu la wapiganaji wa Taliban kwa siku ya tatu mfululizo.

Mashambulizi hayo yalifanyika wakati washika dau wa kimataifa na kikanda wakikutana mjini Brussels pembezoni mwa mkutano unaoendelea na wakikubaliana kuongeza juhudi za kutafuta Amani kati ya serikali ya Afghanistan na kundi la Taliban.

Afisi ya kutoa msaada wa upatanishi unaongozwa na NATO nchini Afghanisan umesema mapema leo kuwa serikali ya Afghanistan ingali inadhibiti mji wa Kunduz na kwamba kuna mapigano ya hapa na pale wakati vikosi vya kitaifa vikiendelea kushikilia udhibiti huo.

XS
SM
MD
LG