Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 18:04

Balozi wa Marekani Libya auawa katika shambulizi



Maafisa wa Libya wanasema Balozi wa Marekani nchini Libya, Christopher Stevens, na wafanyakazi wengine wa ubalozi wameuawa baada ya kundi la watu kuvamia ubalozi mdogo katika mji wa Benghazi Jumanne usiku.

Vifo hivyo vimetokea baada ya waandamanaji waliokasirishwa na sinema iliyotengenezwa Marekani ikimkashifu Mtume Muhammad kufyatulia risasi na kuchoma moto sehemu za ubalozi huo mjini Benghazi.

Balozi J. Christopher Stevens, mwanadiplomasia wa siku nyingi na mmoja wa mabalozi wenye uzoefu mkubwa katika eneo hilo, alikuwa nchini humo chini ya miezi minne tu baada ya kuchukua wadhifa huo mjini Tripoli mwezi Mei.

Waziri mdogo wa mambo ya ndani wa Libya Wanis al-Sharif alisema balozi huyo aliuawa "pamoja na maafisa wengine watatu," akithibitisha kuwa Stevens alikuwepo ndani ya ubalozi huo uvamizi ulipotokea.

Sharif aliwaambia waandishi kuwa kundi la watu wenye silaha walishambulia ubalozi huo katika hali ya "kujitoa mhanga." Alisema ubalozi wa Marekani "una makosa" kwa kutochukua hatua za kutosha. Wizara ya mambo ya nje ya Marekani haijatoa tamko lolote kuhusiana na habari hiyo.
XS
SM
MD
LG