Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 19, 2024 Local time: 17:35

Marekani yaonya kuhusu shambulizi la kigaidi Uganda


Picha ya satalaiti ya uwanja wa Entebbe Uganda, July 3, 2014.
Picha ya satalaiti ya uwanja wa Entebbe Uganda, July 3, 2014.

Ubalozi wa Marekani nchini Uganda umetahadharisha kuhusu uwezekano wa shambulizi la kigaidi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Entebbe huko Uganda.

Ubalozi huo unasema katika ukurasa wake wa internet kuwa kulingana na habari za kipelelezi kuna "tishio mahsusi" kwamba kundi la magaidi wasiojulikana litashambulia uwanja huo wa ndege Alhamisi July 3. Ubalozi huo unasema umepata taarifa zake kutoka jeshi la polisi la Uganda.

Ubalozi umetahadharisha watu wanaopanga kusafiri kupitia uwanja huo kuangalia upya mipango yao ya usafiri kufuatia habari hizi.

Mapema, maafisa katika serikali ya Washington walisema Marekani inapanga kuongeza ulinzi katika baadhi ya viwanja vya ndege nje ya nchi huku kukiwa na wasiwasi kuwa al-Qaida huenda inatengeneza aina mpya ya bomu linaloweza kuingizwa kwa siri ndani ya ndege.

Waziri wa Usalama wa Ndani Jeh Johnson anasema Marekani inaongeza ulinzi katika baadhi ya viwanja vya ndege vya nchi za nje vyenye safari za moja kwa moja kwenda Marekani.

XS
SM
MD
LG