Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:15

Mgogoro wa Sudan Kusini wasababisha uhaba mkubwa wa chakula nchini


Watu wakiwa katika mstari kwenye ugawaji wa chakula katika jimbo la Unity nchini Sudan Kusini.
Watu wakiwa katika mstari kwenye ugawaji wa chakula katika jimbo la Unity nchini Sudan Kusini.

Umoja wa Mataifa unasema idara zake zinasema mgogoro wa Sudan Kusini ukijumuishwa na hali ya hewa umepunguza sana uzalishaji wa chakula nchini humo.

Idara ya Chakula na Kilimo ya Umoja wa Mataifa pamoja na mpango wa chakula duniani (WFP) unasema uzalishaji wa chakula wa Sudan Kusini ni wa chini kuwa tani 400,000 kwa mwaka huu ikiwa ni kushuka kwa asilimia 53 ikilinganishwa na mwaka uliopita.

Hali hii imeendeleza hali mbaya ya upungufu mkubwa wa chakula katika maeneo yote ya nchi. Makadirio haya yanafuatiwa na ripoti kutoka makundi mengine ya misaada ambapo inaelezwa familia zinaidhi kwa kutegemea mlo mmoja tu kwa siku kwa sababu ya kupanda sana gharama za chakula.

XS
SM
MD
LG