Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 10, 2023 Local time: 16:40

Upinzani Zimbabwe waeleza matumaini ya kushinda uchaguzi 2023


Kiongozi wa upinzani nchini Zimbabwe, Nelson Chamisa, akiwasili Masvingo kuhudhuria mkutano wa uchaguzi mdogoto Jumapili, March 20, 2022. (Picha na VOA).
Kiongozi wa upinzani nchini Zimbabwe, Nelson Chamisa, akiwasili Masvingo kuhudhuria mkutano wa uchaguzi mdogoto Jumapili, March 20, 2022. (Picha na VOA).

Kiongozi wa upinzani nchini Zimbabwe Nelson Chamisa ameeleza matumaini kwamba chama chake cha Citizens Coalition for Change, CCC, kitashinda uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.

Hii ni baada ya chama cha CCC kupata theluthi mbili ya viti katika uchaguzi mdogo wa bunge na manispaa licha ya kupitia hali ngumu sana wakati wa kampeni.

Chama hicho ambacho kiliundwa miezi mitatu iliyopita kutoka kwa chama cha upinzani cha Movement for democratic change, MDC, kinaonekana kutoa ushindani mkali dhidi ya chama kinachotawala cha ZANU-PF.

Kimeshinda viti 19 vya bunge kati ya 28.

Uchaguzi huo umefanyika kutokana na vifo, kujiuzulu na kuondoka kwa wabunge wa chama cha MDC.

Chama cha Chamisa pia kimeshinda viti 75 kati ya 122 vya manispaa.

Chamisa anaeleza kuwa: "Tumeshinda kwa idadi kubwa sana ya viti lakini tunasisitiza kwamba kuna hitajika mabadiliko makubwa sana kwa sheria za uchaguzi nchini humu na kuhakikisha kwamba matokeo ya uchaguzi yanatolewa kwa njia nzuri zaidi. Vituo vya kupigia kura havistahili kuwa na ghasia na wapiga kura hawastahili kutishiwa jinsi ambavyo tumeshuhudia.

Uchaguzi huo mdogo ulionekana kama mtihani mkubwa kwa chama chake rais Emmerson Mnangagwa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.

Hakuna chama cha upinzani kimewahi kushinda uchaguzi na kuunda serikali tangu Zimbabwe ilipopata uhuru mwaka 1980.

XS
SM
MD
LG