Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 13, 2024 Local time: 06:09

Upinzani waahidi tuzo ya dola milioni 1 kwa kukamatwa Gadhafi.


Majeshi ya wapinzani Libya.
Majeshi ya wapinzani Libya.

Mapambano makali yanaendelea na wapinzani wawarudisha nyuma askari wa Gadhafi.

Upinzani wa Libya umeahidi kutoa zawadi ya dola milioni 1.67 kwa kukamatwa kwa kiongozi wa Libya Moammar Gadhafi. Ahadi hiyo ya fedha ilitolewa wakati mapigano yalipolipuka tena katika nyumba ya Gadhafi huko Tripoli siku moja baada ya waasi kuchukua jumba hilo.

Mkuu wa baraza la mpito la taifa Mustafa Abdel Jalil amesema kundi lake linaunga mkono uamuzi wa wafanyabiashara wa mji huo kutoa ahadi hiyo katika juhudi za kuharakisha kukamatwa kwa Gadhafi.

Wapiganaji wa upinzani waliwarudisha nyuma waunga mkono wa Gadhafi katika mapigano ya risasi holela leo baada ya kusherekea kuchukua jumba la Gadhafi siku moja kabla. Walichukua silaha,Televisheni na mapambo kwenye eno hilo wakati wakiendelea kumtafuta Gadhafi. Gadhafi hajulikani alipo lakini maafisa wa Marekani walisema jana Jumanne kuwa bado wanaamini kuwa yupo Libya.

XS
SM
MD
LG