Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 29, 2023 Local time: 18:28

Wapinzani Venezuela wajitokeza kwa wingi kuhakiki saini


Wafuasi wa upinzani nchini Venezuela walisubiri katika foleni kubwa mapema leo kuhakiki saini zao.
Wafuasi wa upinzani nchini Venezuela walisubiri katika foleni kubwa mapema leo kuhakiki saini zao.

Wafuasi wa upinzani nchini Venezuela walisubiri katika foleni kubwa mapema leo kuhakiki saini zao ikiwa ni sehemu ya mchakato mkubwa wa kutaka kura ya maoni dhidi Rais Nicolas Maduro.

Maelfu ya watu walijitokeza katika vituo vya ukaguzi nchini mote kwa ajili ya kuchukuliwa alama za vidole ikiwa ni sehemu ya masharti ya Baraza la Uchaguzi ambapo wale wote waliotia saini shauri la kutaka ifanyike kura kurudi katika vituo vya kupigia kura kwa ajili ya kuhakiki saini zao.

Kiongozi wa upinzani aliwasilisha saini milioni 1 kwa kutaka kufanyika kwa kura hiyo, ikiwa ni zaidi ya watu laki mbili waliohitajika ili kuendelea na hatua ya pili.

Upinzani unamlaumu Rais Maduro mwenye sera za kijamaa kwa upungufu wa chakula na dawa na kusababisha mfumuko wa bei na kuongezeka kwa tatizo la umeme la mara kwa mara.

XS
SM
MD
LG