Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 00:12

Upinzani nchini Kenya wasitisha maandamano


Kiongozi wa upinzani Raila Odinga akihutubia wafuasi wake wakati wa maandamano katika mtaa wa Kibera, Machi 27, 2023.
Kiongozi wa upinzani Raila Odinga akihutubia wafuasi wake wakati wa maandamano katika mtaa wa Kibera, Machi 27, 2023.

Upinzani nchini Kenya Jumatano ulitangaza kwamba umesitisha duru nyingine ya maandamano yaliyopangwa dhidi ya serikali katika kile kinachoonekana kama hatua ya kutafuta njia ya kuanzishwa tena kwa mazungumzo ya pande mbili yaliyokwama kuhusu mzozo wa kisiasa unaoendelea.

Wafuasi wa kiongozi mkongwe wa upinzani Raila Odinga walifanya maandamano kadhaa tangu mwezi Machi wakidai uchaguzi wa rais wa mwaka jana uliibiwa, na pia kwa kile anasema ni kushindwa kwa serikali kukabiliana na kupanda kwa gharama ya maisha.

Muungano wa kisiasa wa Odinga, Azimio la Umoja ulikuwa umepanga kufanya maandamano mengine leo Alhamisi, lakini umesema katika taarifa kwamba uongozi wake umekubaliana kusitisha mpango huo.

Serikali ya Rais William Ruto ilitoa wito wa mazungumzo ya pande mbili kujaribu kutatua mzozo huo, lakini mchakato huo ulikwama kutokana na malumbano kadhaa.

Azimio imesema kuwa imewaita wajumbe wake wa mazungumzo kujadili “ushiriki zaidi” na muungano wa Ruto wa Kenya Kwanza.

“Tungependa kusisitiza pia kwamba hatutasita kuanzisha maandamano makubwa kukiwa na ishara yoyote ndogo ya ukosefu wa nia njema na uaminifu upande wa Kenya Kwanza,” muungano wa azimio umesema.

XS
SM
MD
LG