Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 30, 2024 Local time: 21:18

Upinzani Ghana kufungua mashtaka dhidi ya tume ya uchaguzi


Kiongozi wa upinzani wa NPP nchini ghana, Nana Akufo-Addo
Kiongozi wa upinzani wa NPP nchini ghana, Nana Akufo-Addo

Wanasheria wa chama cha upinzani nchini Ghana cha National Democratic party-NDP wanapanga kufungua kesi mahakamani katika mji mkuu Accra siku ya Alhamis wakitoa changamoto kufuatia uamuzi wa tume ya uchaguzi kutomuidhinisha mgombea urais wa chama chao Nana Konadu Agyemeng Rawlings ambaye ni mke wa rais wa zamani nchini humo kushiriki katika uchaguzi mkuu wa Disemba saba.

Katibu mkuu wa NDP, Mohammed Frimpong alisema kutolewa jina la mgombea huyo kunaonekana kuchochewa kisiasa ili kuhakikisha bibi Rawlings haweki kitisho chochote kwa rais aliyeko sasa madarakani John Dramani Mahama wa chama tawala cha National Democratic Congress-NDC ambaye anatarajiwa kukabiliana na changamoto kutoka kwa kiongozi mkuu wa upinzani, Nana Addo Dankwa Akufo-Ado wa chama cha New Patriotic Party-NPP.

XS
SM
MD
LG