Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 15, 2024 Local time: 06:04

Upinzani Afrika Kusini wakosoa shirika la SABC


Julius Malema, kiongozi wa chama cha upinzani cha Economic Freedom Fighters (EFF).
Julius Malema, kiongozi wa chama cha upinzani cha Economic Freedom Fighters (EFF).

Julius Malema, kiongozi wa chama cha upinzani cha EFF alisema kukataliwa kwa tangazo la kampeni la chama chake kunahujumu mchakato wa uchaguzi mkuu ujao.

Shirika la serikali la utangazaji nchini Afrika kusini-SABC limeshutumiwa vikali na chama cha upinzani cha Economic Freedon Fighters-EFF kwa kutumia kile chama hicho kinasema ni mbinu zinazofanana na zile za enzi za ubaguzi wa rangi kwenye matangazo yake.

Lawama hizo zinafuatia hatua ya SABC kukataa kupeperusha tangazo la chama hicho cha kisiasa kama sehemu ya kampeni zake kabla ya uchaguzi mkuu wa Mei 7.

Julius Malema, kiongozi wa chama hicho cha EFF ambaye zamani alikuwa kiongozi wa vijana katika chama tawala cha African National Congress (ANC), alisema kukataliwa kwa tangazo la chama chake cha kisiasa kunahujumu mchakato wa uchaguzi ujao.

Chama cha EFF kitashiriki kwa mara ya kwanza kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
XS
SM
MD
LG