Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 08, 2022 Local time: 01:37

Watu wachache wajitokeza kupiga kura Kenya


Waandishi wa Sauti ya America katika miji mbali mbali ya Kenya wanasema idadi ya wapiga kura ni ndogo kulingana na uchaguzi uliyopita.

Marudio ya uchaguzi wa rais yafanyika Kenya
please wait

No media source currently available

0:00 0:04:10 0:00

Vituo vya upigaji kura vilifunguliwa katika sehemu nyingi za nchi ingawa kuna baadhi ya vituo katika miji ya Kisumu, Nairobi na Mombasa vilikabiliwa na upinzani.

Polisi walilazimika kutumia mabomu ya kutoa machozi katika kitongoji kikubwa cha Nairobi cha Kibera ili kutawanya watu walokua wamefunga njia za kuelekea katika vituo vya kupiga kura.

Katika ngome za mungano wa upinzani wa NASA waandishi wetu wanaripoti kutokuwepo na wapiga kura hasa huko Kisumu baadhi ya wananchi walisema kuwa hawapigi kura kutii wito wa kiongozi wao Raila Odinga.

Maafisa wa usalama nje ya kituo cha Kinyanjui Nairobi bila ya wapiga kura
Maafisa wa usalama nje ya kituo cha Kinyanjui Nairobi bila ya wapiga kura

Katika mji wa Gatundu anakotoka mgombea wa chama tawala Rais Uhuru Kenyatta kwa mujibu wa mwandishi wa VOA mpaka saa moja asubuhi foleni ilikuwa ni fupi na watu wachache kujitokeza, tofauti kabisa na ilivyokuwa wakati wa uchaguzi wa Ogosti 8.

Mmoja wa wakazi wa eneo waliokuwa kwenye foleni ya kupiga kura alisema mvua iliyonyesha asubuhi ni sababu ya watu kutojitokeza mapema siku hiyo akitarajia watu wataongezeka siku kadri itakavyokuwa inaendelea.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG