Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 03, 2023 Local time: 20:14

Kura ya Uingereza kujitoa EU yaendelea


Upigaji kura wa kihistoria unaendelea leo nchini Uingereza wa kuamua iwapo nchi hiyo itabaki kwenye Muungano wa Ulaya au LA.

Wakati shughuli hiyo ikiendelea, ushindani mkubwa umedhihirika miongoni mwa wapiga kura. Wapiga kura wanatarajiwa kujitokeza kwa wingi baada ya kampeni kali iliochukua miezi miwili ikiangazia zaidi swala la uhamiaji ambalo katika siku za karibuni limekuwa nyeti wakati taifa hilo likishuhudia ongezeko maradufu la wahamiaji tangu 2000.

Katika dakika za mwisho mwisho za kampeni, Waziri Mkuu David Cameron amehimiza umuhimu wa kubaki kwenye muungano huo akisema ni bora Uingereza kuwa ndani ya Muungano wa Ulaya uliofanyiwa marekebisho.

Cameron pamoja na wengine wanaopinga wazo la kujiondoa kwenye muungano huo wanasema kuwa uchumi wa Uingereza utaathiriwa pakubwa iwapo itajiondoa.

XS
SM
MD
LG