Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 02:17

Wanafunzi waliojeruhiwa Arusha wafanyiwa upasuaji Marekani


Mbunge Nyalandu
Mbunge Nyalandu

Upasuaji uliofanywa kwa wanafunzi majeruhi wa shule ya Lucy Vincent ya mkoani Arusha, Tanzania umeenda vizuri nchini Marekani.

Wanafunzi hao wanatibiwa katika hospitali ya Mercy jijini Sioux katika jimbo la IOWA nchini Marekani na hali zao zinaendelea vizuri.

Majeruhi Sadya Awadh na Wilson Tarimo wote walifanyiwa upasuaji jana wakati Doren Mshana alifanyiwa juzi kwa mujibu wa vyanzo vya habari nchini Marekani.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kupitia gazeti la Habari Leo Tanzania, Mbunge wa Singida Kaskazini na rafiki wa karibu wa watalii madaktari waliowaokoa majeruhi na kuopoa maiti siku ya ajali Mei 6, mwaka huu.

Ajali hiyo ilitokea katika eneo la kilima cha Rhotia, Karatu na kusababisha vifo wanafunzi 32 wakiwemo walimu wawili wanafunzi na dereva, aliandika hayo katika ukurasa wake wa Facebook jana.

Hata hivyo Lazaro Nyalandu alisema: “Kila mtoto amewekwa kwenye chumba chake peke yake, na mama mzazi na muuguzi mmoja wanakuwa naye wakati wote.” Mbunge huyo alisema Sadya amefanyiwa upasuaji maeneo matatu yaliovunjika ikiwemo mkono wa kulia lakini shingo haikufanyiwa upasuaji na badala yake aliwekewa kifaa cha kunyoosha (Brace) atakayokaa nayo wiki sita kuanzia sasa.

“Wote wanaendelea na mapumziko katika hospitali ya Mercy, Sioux City. Mungu ni mwema sana,” aliandika Nyalandu.

XS
SM
MD
LG