Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 08:17

Uongozi wa Korea Kaskazini hautetereki licha ya vikwazo vya UN


Afisa wa Korea Kusini anasema kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un, akiendeleza kuongeza nguvu zake kwa hivi sasa anaonekana hatetereki kufuatia nchi yake kufanya majaribio ya nyuklia ya hivi karibuni na uzinduzi wa roketi zake.

Afisa huyo akiongea kwa masharti ya kutotambulishwa, amesema pamoja na kuondolewa kwa maafisa wake wa ngazi ya juu, ikijumuisha kunyongwa kwa mjomba wa Kim, Jang Song Thaek, mwaka 2013 na kuondolewa kwa waziri wa ulinzi Hyon Yong Chol hapo mwaka jana, hakuna ishara yoyote ya kuongezeka hali ya kutetereka katika uongozi wa Korea Kaskazini.

Afisa huyo ameendelea kusema kadri vikwazo vya kimataifa vilivyowekwa hivi karibuni kuwa vigumu, vinaonekana kutoteteresha uongozi na nguvu ya Korea Kaskazini.

XS
SM
MD
LG